FAHAMU JINSI YA KUTUMIA MBINU YAKINIFU ZA USHAURI-NASIHI KUSAIDIA KUTATUA MATATIZO NA CHANGAMOTO ZA MAISHA YA WATU WA KADA TOFAUTI TOFAUTI
FAHAMU JINSI YA KUTUMIA MBINU YAKINIFU
ZA USHAURI-NASIHI KUSAIDIA KUTATUA MATATIZO NA CHANGAMOTO ZA MAISHA YA WATU WA
KADA TOFAUTI TOFAUTI
Na Mwl. Juma
Rununu:
+255762957992
Barua pepe: jumapeter399@gmail.com
Moshi-Tanzania.

Katika jamii nyingi watu wamekuwa wakiwasaidia wengine kujinasua na matatizo yanayowakabili. Ni jambo lisiloepukika, kwa wakati mwingine tunahitaji msaada kutoka kwa watu wenye uzoefu na uelewa mpana kuwashirikisha kutusaidia tubaini njia chanya za kujinasua kutoka katika matatizo yanayotukumba (stressing problems) kama vile kufanya maamuzi yanayohusu maisha.
Kiukweli ushauri-nasihi umekuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku lakini
hatuna budi kujua kwanini tunauhitaji? Na lipi ni chaguo zuri zaidi?.
Tangu miongo na miongo maana ya istalahi “Ushauri” yaani kwa kiingereza “advice” imekuwa ikichanganywa sana na fasili ya “Ushauri-nasihi” ambayo kwa kiingereza “counselling” kutokana na mpaka finyu usioonekana dhahiri wa kimaana baina ya istalahi hizi mbili zinazokonyezana na kunyatiana. Lakini nikuambie hakika kuwa Ushauri na Ushauri-nasihi ni istilahi mbili zinazoonekana kushabihiana kimofolojia (kiumbo) lakini zina maana tofauti kiutendaji katika muktadha wa maisha yetu katika kutafuta masuluhisho ya matatizo yanayotuandama kila kukicha.
Tangu miongo na miongo maana ya istalahi “Ushauri” yaani kwa kiingereza “advice” imekuwa ikichanganywa sana na fasili ya “Ushauri-nasihi” ambayo kwa kiingereza “counselling” kutokana na mpaka finyu usioonekana dhahiri wa kimaana baina ya istalahi hizi mbili zinazokonyezana na kunyatiana. Lakini nikuambie hakika kuwa Ushauri na Ushauri-nasihi ni istilahi mbili zinazoonekana kushabihiana kimofolojia (kiumbo) lakini zina maana tofauti kiutendaji katika muktadha wa maisha yetu katika kutafuta masuluhisho ya matatizo yanayotuandama kila kukicha.
Ikumbukwe kuwa kila mtu anaweza akawa mshauri na si mshauri-nasihi.
Ushauri-nasihi(Counselling):
Huu ni uhusiano wa kitaalamu unaoanzishwa kati ya mtu mwenye taaluma ya
kiushauri (counsellor) na mtu anayetafuta msaada kutatua tatizo/matatizo yake
binafsi (client). Ushauri-nasihi hujenga uhusiano ambao humsaidia mtu
anayetafuta msaada kupata picha ama mwanga kuhusu tatizo lake ili aweze
kujichagulia njia stahiki ya kutatua tatizo lake mwenyewe.
Mshauri-nasihi ni mtu mwenye taaluma ya kutoa huduma za ushauri-nasihi kwa
watu wanaomjia wakihitaji msaada wa kutafuta mbinu chanya za kujinanua kwenye
matatizo kwa kumshirikisha mtaalamu. Mtaalamu huyu amefundishwa mbinu za kutoa
ushauri-nasihi kwa watu kwa kutengeneza uhusiano wa kitaalamu kati yake na mtu
anayetafuta kusaidiwa ama kupewa mwanga kuhusu tatizo linalomsibu na kumsaidia
mhanga wa tatizo atambue na kujichagulia suluhisho la tatizo/matatizo yake
miongoni mwa masuluhisho mengi.
Kupitia Ushauri-nasihi mahusiano hujengwa na mambo makuu matatu:
●Mshauri-nasihi amwelewe kwa kina mtu anayemwambia
matatizo/shida zake na pia mshauri-nasihi ajiweke katika nafasi ya mhanga wa
tatizo kana kwamba limempata yeye.
●Mhanga wa tatizo aeleze tatizo lake kwa mshauri-nasihi
kwa ukweli wote pasina kupindisha. Pia mshauri-nasihi anapaswa kuwa mkweli.
●Mshauri-nasihi hapaswi kumkosoa, kumlalamikia, kumdharau
wala kumwuuliza mhanga maswali mengi ya kwanini amefanya makosa
yaliyomsababisha ajiingize kwenye matatizo (unconditional acceptance and
avoiding of judgement).
Ili ushauri-nasihi uweze kuwa na tija, mhanga wa tatizo hakuna budi
amwamini mshauri-nasihi na hivyo kujisikia huru kuongea mambo yake binafsi kwa
uwazi bila kuficha kinachomsibu pasipo kuogopa kukosolewa. Mhanga wa tatizo
anapokuwa wazi kuongea mambo yake binafsi, matokeo yake atasaidiwa na
mshauri-nasihi kupata picha/mwanga kuhusu tatizo lake kwa upana na namna ya
kulitatua. Haimaanishi kwamba kupitia ushauri nasihi utatatua tatizo lako moja
kwa moja kwani si mara zote tatizo fulani linaweza kutatuliwa badala yake
humleta mhanga wa tatizo kwenye njia stahiki kutafuta masuluhisho yao wenyewe
kutatua tatizo. Hapa inategemeana na aina ya tatizo.
Ushauri-nasihi yakinifu hautatui tu tatizo la mhanga lakini;
●Husaidia kuondoa/kupunguza matokeo hasi ya tatizo.
●Humwezesha mhanga wa tatizo awe hodari kupambana na tatizo na si
kulikimbia.
●Husaidia kuongeza uvumilivu katika hisia za mhanga wa tatizo.
●Husaidia kurejesha kujiamini na kuondoa baadhi ya vichocheo vya matatizo.
Ushauri(Advice):
Hiki ni kitendo cha kutoa mapendekezo kwa mtu mwingine kwa kumwambia
anachopaswa kufanya ili atatue tatizo/matatizo yake. Asilimia kubwa ya watu
huwa tunatoa ushauri/mapendekezo kwa watu wengine kwa kuwachagulia masuluhisho
ya matatizo yao jambo ambalo ni hatari sana na hatuna budi kuliepuka.
Tunapaswa kutoa ushauri tu pale ambapo tuna uhakika 100% utafanya kazi
kuleta matokeo chanya.
Kwanini hatupaswi kutoa ushauri?
●Tuna uelewa finyu kuhusu tatizo la mhanga.
●Hatutaki kuhusishwa kwa matokeo hasi ya ushauri wetu.
●Inaumiza sana kutoa ushauri usiofanyiwa kazi na mhanga wa
tatizo.
NB: Badala yeke tunawasaidia watu kuzikabili changamoto zao
wenyewe, kuwasaidia waelewa hisia zao na kuwasaidia wajichagulie masuluhisho
yanayoonekana ni bora kwao kutatua matatizo yanayowakumba.
HIZI NI MBINU YAKINIFU UNAZOPASWA KUZITUMIA WAKATI WA KUTOA USHAURI-NASIHI
KWA MTU MWENYE TATIZO
1. Mbinu ya Mawasiliano (communication skill)
Mawasiliano mazuri hutokea pale ambapo kuwa ukweli wa jambo linalozungumzwa (genuine), ubadilishanaji mzuri wa habari kati ya mhanga wa tatizo (sender) na mshauri-nasihi (receiver). Wanapaswa kutazamana machoni, wakati wa mazungumzo hawapaswi kuegemea kitu chochote, ubize wa kushika shika simu hautakiwi na isitokee mmoja anaongea sana kuliko mwingine.
Mawasiliano mazuri hutokea pale ambapo kuwa ukweli wa jambo linalozungumzwa (genuine), ubadilishanaji mzuri wa habari kati ya mhanga wa tatizo (sender) na mshauri-nasihi (receiver). Wanapaswa kutazamana machoni, wakati wa mazungumzo hawapaswi kuegemea kitu chochote, ubize wa kushika shika simu hautakiwi na isitokee mmoja anaongea sana kuliko mwingine.
Mawasiliano mazuri katika mchakato huu humsaidia mhanga wa tatizo kujihisi
ana thamani na huru kutokana na kupewa nafasi ya kusikilizwa, atahisi
kujiamini, ataongeza imani kwa mshauri-nasihi wake, atakuwa tayari kuongea kwa
uwazi mambo binafsi pasipo hofu na kumwongezea uwezo wa kupata picha pana
kuhusu tatizo lake.
Mshauri-nasihi anapaswa kusikiliza kwa makini kwa kuzingatia ishara za
mwili (physical), hisia(emotional), na akili (cognitive/mental) katika
mazungunzo. Tafiti zinaonesha kuwa 80% ya mawasiliano huhusisha mwonekano na
viungo vya mwili.
Mawasiliano hayatakuwa mazuri endapo mshauri-nasihi ataanza kurukia rukia
jambo kabla halijamalizwa kusemwa na mhanga wa tatizo, kuchagua mambo ya
kusikiliza, kukatiza na kumalizia sentensi za mtu anayezungumza, kuanza
kumkosoa sana mhanga wa tatizo, kupotezea baadhi ya mambo yanayozungumzwa.
Mhanga akiona tu mshauri-nasihi anafanya baadhi ya mambo haya lazima
ataacha kumwamini na hataongea ukweli wa mambo yake binafsi.
2. Mbinu ya kuuliza maswali(questioning
skill)
Mbinu hii humsaidia mhanga wa tatizo
kuelezea mkasa kwa undani ili kumfanya mshauri-nasihi kuelewa kisa kwa kina.
Mshauri-nasihi anapaswa kuzingatia mambo ya msingi wakati wa kumwuuliza
mhanga wa tatizo. Mambo hayo ni kama vile; swali moja libebe kitu kimoja tu,
atumie lugha rahisi yenye kueleweka kwa mhanga, aepuke maswali mengi kwa wakati
mmoja, aepuke kudakia dakia wakati swali bado linajibiwa, aepuke kuuliza
maswali ya kwanini, mtindo uwe wa
swali-jibu.
3.
Rejea hoja/sentensi muhimu zilizozungumzwa na mhanga wa tatizo(Paraphrasing)
Wakati unazungumza na mhanga gusia baadhi ya sentensi alizozisema wakati
umemsikiliza kama sehemu muhimu ya kujua pa kuanzia kumsaidia. Hii inamfanya
mhanga ajisikie vizuri kwani wakati unarejea alichozungumza atakuamini zaidi
kwamba ulikuwa makini kumsikiliza yeye na shida zake.
Mfano; “Kama nimeelewa
umesema......”, “Kwahiyo unasema.....”, “kwahiyo unamaanisha kwamba......”.
4. Mbinu ya kulenga kinachosemwa na
kumaanishwa na si mengine(Focusing skill)
Fanya mawasiliano yawe mahususi na si jumuishi juu ya uhakika na hisia za
mhanga kuhusu anayoyazungumzwa kujua tatizo limemgusa na kumuumiza kwa namna
gani. Mshauri-nasihi anapaswa kuepuka kauli jumuishi, kauli zinazogusa imani ya
mtu bali mazungumzo yalenge kusaidia utatuzi wa kiini cha tatizo na si
vinginevyo.
Msaidie mhanga wa tatizo kutambua kiini cha tatizo na kuegemea hapo na si
mengine yasiyohusiana na tatizo, tumia maswali kusaidia mhanga atoe ufafanuzi
wa hisia na lengo lake. Ikumbukwe watu wengine wenye matatizo husimulia mikasa
mingi kwa wakati mmoja hapo tufanye nini? Na ushauri-nasihi unasidia kutatua
tatizo moja moja. Mshauri-nasihi anaweza kusema yafuatayo kwa kumwambia mhanga
“Hapa sasa hebu kwa leo tuanza na jambo
hili kwanza halafu tutaenda na mengine pia pole sana nasikitika kukuona upo
kwenye hali ya huzuni yatakwisha tu usijali”. Mbinu hii itamrudisha mhanga
wa tatizo kwenye hoja mahususi.
5. Mbinu ya kutunza siri za mtu
aliyekuambia matatizo yake.
Wengi wetu tumekuwa tukivujisha siri za watu wanaotuamini na kutuambia
mambo na matatizo yao binafsi. Hii inatufanya tusiaminike na watu wasiwe tayari
kutushirikisha mambo yao binafsi kwani wanatuhofia tunaweza kusambaza umbea
kuhusu wao. Mshauri-nasihi aliyekula kiapo cha kutoa huduma za kishauri-nasihi
kwa watu hayuko tayari kuvujisha siri ya mteja wake hata kwa mpenzi wake
anayemwamini.
Uhusiano wa kuaminiana na mhanga wa tatizo ni kuwa mshauri-nasihi anapaswa
kumhakikishia mhanga kuwa yote yatakayojadiliwa yatabakia kuwa siri ya wawili.
Swali la kujiulizwa je, ni kwa namna gani anayetaka kunieleza matatizo yake
aniamini kuwa itabakia kuwa siri na hakuna yeyote asiyehusika atajua
kilichojadiliwa? Ni kupitia mambo yafuatayo;
●Kusaini fomu maalumu ya uhakikisho kabla ya mjadala kuwa chochote
kitakachozungumziwa kitabakia kuwa siri ya wawili. Endapo mshauri-nasihi ataivujisha
siri atashitakiwa kisheria kwa kosa la kuvunja mashariti ya mteja wake.
●Mshauri-nasihi atatoa uhakikisho kwa mdomo mbele ya mhanga wa tatizo kuwa
siri haitavuja.
●Mshauri-nasihi aepuke kutumia mifano ya wahanga wengine wa matatizo kama
mifano wakati akiongea na mtu aliyekuja kwake kupata msaada wa kishauri-nasihi
kwa ajili ya kutatua tatizo lake.
Siri inaweza kuvujishwa makusudi kwa sababu zifuatazo;
●Endapo mhanga wa tatizo atakapoongea maneno ya kutishia usalama wa yeye
binafsi, mtu aliyemkosea ama jamii inayomzunguka. Hapo kama wewe ni
mshauri-nasihi unatakiwa uwakimbilie askari polisi wamkamate mhanga wa tatizo
kwani anahitaji kuvuruga amani na si kutatua tatizo.
●Endapo mhanga wa tatizo ana umri chini ya miaka 18 na amekuwa mhanga kwa
kubakwa, unyanyasaji wa mtoto/watoto na namna zingine za uhalifu.
Na Mwl. Juma
Mwandishi wa makala mbalimbali kwa jamii.
No comments